Saturday, December 25, 2010

MAISHA NI SAFARI

    MAISHA YANGU YAMEKUWA KATIKA MTIRIRIKO NA CHANGAMOTO NYINGI SANA: Kwa  mwanadamu yeyote ambaye ana akili timamu ni wazi ataweza kukumbuka mambo mengi maishani mwake,  kuna matukio ya furaha na huzuni, wakati mwengine inakuwa vigumu kuona uhalisia wa mambo yajayo mbele, lakini kwa ujumla mwanadamu anapaswa kuwa na kumbukumbu ya historia yake maishani.Hili ni jambo muhimu na linapaswa kuzingatiwa kwa bidii. nchi yetu imeshindwa kuhifadhi historia za kweli za mashujaa wetu. nchi imechukuliwa na sahau,  mwandishi  SHAABAN ROBERT  aliliona hili mapema ukisoma  riwaya yake ya WASIFU WA SITY BINT SAAD utaona ukweli wa uzembe huu tulionao.                GEORGE LILANGA bado historia yake haijakamilika hata theluthi moja.  SWALI; Ni kweli HENDRICK LILANGA mjukuu wake atahitimisha mdahalo unaoendelea sasa juu ya historia ya kweli ya babu yake?    jee kitabu anachokiandaa sasa kuhusiana na  historia ya maisha ya babu yake kitaushangaza ulimwengu?  au nini tutegemee.  TUSUBIRI TUONE.

1 comment:

  1. INAWEZEKANA KUPTA HISTORIA YA KWELI YA GEORGE LILANGA, LAKINI INAHITAJIKA BIDII NA UDADISI IKINIFU.

    ReplyDelete